Back to top

Muliro kuwashughulikia wanaowapa mimba wanafunzi na kukatisha masomo.

26 November 2020
Share

Vyombo vya Dola Mkoani Mwanza vimetangaza vita dhidi ya watu wanaoendelea kujihusisha na vitendo vya ukatili wa jinsia, ikiwemo kuwashughulikia kwa nguvu zote wanaowapa mimba wanafunzi na kukatisha ndoto zao za maisha.

Vita ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto imetangazwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Bwana Muliro Jumanne Muliro wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia, yaliyofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.