Back to top

Mume mbaroni kwa kumjeruhi mkewe kushinikiza kupewa faida ya mgahawa.

11 October 2018
Share

Mkazi wa kijiji cha  Kyamwame wilayani Rorya Bi. Veronica Moga,amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara baada ya kupigwa kwa kutumia mpini wa jembe, panga, kigoda na kumchapa viboko na mtu ambaye ametajwa kuwa ni mume wake wa ndoa wakati akishinikishinikiza kupewa faida iliyopatikana katika mgahawa wake.


Akizungumza wakati akipatiwa matibabu wodi namba nne katika hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Mara, mwanamke huyo amesema amepata kipigo hicho baada ya kumweleza mume wake huyo kuwa sehemu ya faida ya mgahawa amelipa deni la mfuko wa ngano, kitendo kinachodaiwa kumchukiza mumewe na kuanza kumshambulia,Jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime Rorya,wilaya ya polisi ya Kinesi,limeithibisha kumshikilia mtuhumiwa huyo.