Back to top

Museveni akanusha kujeruhiwa kwa Bobi Wine, avilaumu vyombo vya habari

20 August 2018
Share

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekanusha kwamba mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amejeruhiwa huku akilaumu watu maalum ambao ameeleza kuwa ni wa nje wanaotafuta kuingilia siasa za nchi hiyo.

Katika taarifa yake ya kwanza kuhusu afya ya mbunge huyo aliyekamatwa na vikosi vya usalama nchini humo, Museveni amevishutumu vyombo vya habari kwa kile alichokitaja ni kueneza habari zisizo za kweli kuhusu suala hilo.

Museveni amesema  amewasiliana na madaktari wa jeshi, kwasababu ya nidhamu ya jeshi, madaktari wa UPDF daima wanachukua tahadhari katika hali kama hizi ambao wamemuarifu kuwa Hakuwa na majeraha ya kichwa, kifua au mifupa kuvunjika.

Chama cha wafanyakazi wa afya nchini Uganda kimesema mahali wanapohifadhiwa wabunge wa upinzani na vyombo vya usalama akiwemo BOBI WINE ni ya hatari na inaweza kuwasababishia vifo Viongozi wa chama hicho wakisema kuwa madaktari wa Jeshi LA UPDF hawana ujuzi wa kutosha kuwafanyia matibabu wabunge hao wanaodaiwa kujeruhiwa vibaya na maafisa wa usalama.

Wameongezea kuwa mbunge Francis Zake ambaye ni miongoni mwa waliokamatwa yuko katika hali mahututi na anahitaji kuhamishwa kutoka hospitali moja hadi nyingine kupata matibabu ya hali ya juu.