Back to top

Muswaada wa bima ya afya kuwasilishwa bungeni.

19 April 2021
Share

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia , wazee na watoto imesema inatarajia kuwasilisha bungeni muswaada wa bima ya afya kwa wananchi wote hapa nchini mwezi June mwaka huu baada ya kukamilisha mchakato wa kupokea maoni mbalimbali kwa wadau wa afya na kuwa na sheria bora.

Naibu Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dokta Godwin Moleli ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mhe Janeth Elias aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wajasirimali wadogo kupata bima ya afya kupitia vikundi vya pamoja.

Dokta Moleli amesema dhamira ya serikali ni  kuhakikisha kila mwananchi anapata matibabu kupitia bima ya afya mpango utakaohusika kila mwananchi baada ya muswaada huo kukamilika baada ya kuwasilishwa bungeni kujadiliwa na wabunge na baadae kuwa sheria baada ya bunge kupitishwa muswaada huo wa  bima ya afya kwa kila mwananchi na kuwa sheria.

Naibu waziri huo wa afya amesema mpaka sasa jumla ya vikundi elfu 32, 343 vimesajili kupata huduma ya afya kupitia mfumo wa vifurushi vya bima ya afya mpango ambao unaendele kwa sasa kote nchini.

Wakati huo huo Dokta Moleli amesema serikali ina mpango endelevu wa kutoa elimu kwa wananchi wakiwemo wachimbaji wadogo na wakubwa katika migodi juu ya  matumizi ya kemikali aina ya zebaki ambayo imekuwa ikisababisha madhara kwa wananchi kutokana na kutokuwa na elimu ya matumizi ya kemikali hizo kwa sasa.