Back to top

Mwakyembe asema ndani ya dakika 10 sakata la Morrison analimaliza.

12 August 2020
Share

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amesema mwenendo wa sakata la Morrison linavyoendelea endapo likifanikiwa kufika mezani kwake ndani ya dakika 10 tu anakuwa ameshalimaliza.

"Kitu gani kinawapa shida TFF kukaa mpaka mnashikana mashati siku mbili tatu, wakati kitu kinachoeleweka ni kwamba, kwanza kuna mkataba?, ulikwenda wapi mkataba kama upo mtu anasema tu maneno fanya maamuzi, sasa unavyo zidi kuchelewesha ndio maana watu wengine wanasema shida viongozi wetu wa michezo ni washabiki wa vyama"Amesema Mwakyembe.

Bernard Morrison

Via Clouds Digital.