Back to top

Mwakyembe awaonya watu wanao piga picha na kusambaza mtandaoni.

09 July 2019
Share

Waziri wa Habari Dkt.Harisson Mwakyembe ametoa onyo kwa watu wanaopiga picha za ajali na kuanza kusambaza mtandaoni.

"Watanzania nawaomba sana hebu tuendeleze utamaduni wetu wa utu, ndugu zetu wanapopata ajali nawaomba sana acheni kabisa hii tabia ya kuchukua picha na kurusha kwenye mitandao, nakuanzia sasa hatutaongea tena"-Dkt.Mwakyembe.

Dkt.Mwakyembe ametoa kauli alipokuwa Makao Makuu ya Azam Media alipofika kutoa pole na kisha kuungana na waombolezaji kwenye zoezi la kuwaaga wafanyakazi watano wa Azam media waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Singida.

Amebainisha kwamba sheria ya makosa ya mtandao inazuia chini ya kifungu cha 23, hivyo anaona kinachoendelea ni utamaduni mpya wa binadamu bila kufikiria kitendo cha kupiga picha na kutuma mtandaoni kwamba watu hao wanandugu, wanamarafiki na watoto.