Back to top

Mwalimu Kizimbani kwa kuomba rushwa ya Ngono kwa mwanafunzi.

18 September 2021
Share

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Mbarali mkoani Mbeya imemfikisha Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nyeregete Adelhade Mijindo katika mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake, ili amsaidie kufaulu mtihani wa taifa wa darasa la saba.
.
Imedaiwa kuwa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa manafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, taasisi hiyo iliandaa mtego uliofanikisha kumnasa mwalimu akiwa na mwanafunzi wake ndani ya moja ya vyumba vya nyumba moja ya kulala wageni katika mji mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali na baada ya kupata kibali cha Mwendesha Mashtaka wa Serikali mtuhumiwa amefikishwa mahakamani.
.
Mwalimu huyo amesomewa shitaka la kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake ambalo amelikana.
.
Licha ya dhamana kuwa wazi, mtuhumiwa amepelekwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza sharti linalomtaka awe na wadhamini wawili wenye barua kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji.
.
Mheshimiwa Hakimu Teddy Mlimba ameliahirisha shauri hilo hadi Septemba 28, mwaka huu litakapotajwa tena mahakamani hapo.