Back to top

Mwanafunzi afariki baada kucharazwa bakora na mwalimu Ruvuma.

19 July 2021
Share


Watu 5 wamefariki dunia ndani ya siku 7 katika matukio tofauti mkoani Ruvuma likiwemo la mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya sekondari Mbinga wilayani Namtumbo kufariki dunia baada ya kupigwa viboko na walimu wake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Joseph Konyo amesema wanawashikilia walimu sita kutokana na kifo cha mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 15 ambaye hajamtaja jina kwa sababu za uchunguzi.

Katika matukio mengine Kamanda Konyo amesema mzee wa miaka 85 mkazi wa Kijiji cha Marungu Wilayani Nyasa aligongewa mlango na alipofungua mtu asiyefahamika aliingia ndani na kumvuta chini kutoka kitandani na kumkata kwa shoka na katika tukio lingine la mauaji  limetokea Wilayani Mbinga, ambapo mtu mmoja ameuawa kwa kukatwa miguu kwa tuhuma za wizi wa kuku.