Back to top

Mwanafunzi afariki kwa kufukiwa na kifusi Chato.

17 September 2020
Share

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maweni Wilayani Chato Mkoani Geita, Swaumu Hasan mwenye umri wa miaka kumi na miwili amefariki dunia na  wengine watano wame jeruhiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakitekeleza adhabu ya kuchimba mchanga waliopewa na mwalimu mkuu wa shule hiyo.

ITV ilifika eneo la tukio na kushuhudia mamia ya wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi na jeshi la zimamoto na uokoaji   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Bwana Mtatiro Kitinkwi amethibisha tukio hilo.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika shule hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amelifunga eneo hilo hatarishi.

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho ameagiza kukamatwa kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo anayedaiwa kutoroka.