Back to top

Mwanafunzi Geita auawa kwa kutuhumiwa kuiba shilingi elfu 12.

09 April 2021
Share

Mtoto yatima Method Hasani mwenye umri wa miaka kumi na mbili  mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Kalangalala mkoani Geita ameuawa na jirani yake kwa kushambuliwa na bomba kichwani akimtuhumu kumuibia shilingi elfu kumi na mbili katika duka lake.
.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Henry Mwaibambe amesema jeshi hilo linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Hamadi Juma ili kumfikisha mahakamani.