Back to top

Mwanafunzi Kenya akutwa na dalili za Corona.

03 February 2020
Share

Mwanafunzi mmoja amelazwa katika chumba maalam katika hospitali ya rufaa ya Coast General jijini Mombasa Pwani ya Kenya, baada ya kuonyesha dalili ya kumbukizwa virusi vya maradhi ya Corona.


Mwanafunzi huyo  anayefahamika kama Shukri Jamal Mahmood, ni mkaazi wa eneo la Likoni hapa Mombasa, aliwasili Mombasa kutoka Uchina tarehe 30 mwezi uliyopita, taifa ambalo anasomea udaktari katika chuo kikuu cha Gaunzou.


Mwanafunzi huyo aliwasili katika hospitali ya Coast General baada ya kuonyesha dalili za virusi vya Corona.