Back to top

Mwanaume mmoja auawa baada ya kupigwa Risasi na Askari Mkoani Kagera.

21 May 2018
Share

Mkazi wa kijiji cha Bubare kilichoko katika kata ya Kakungu iliyoko wilayani Misenyi mkoani Kagera Josephat Joseph ameuwawa  kwa kupingwa risasi  na askari waliokuwa kwenye harakati za kuokoa maisha yao baada ya kuvamiwa  na kundi la wafugaji waliotaka kuwanyanganya Ng’ombe zaidi ya 300 waliokamatwa ndani ya katika kitalu namba 20 cha mwekezaji wa kampuni ya Farmers  Investment alichomilikishwa na kampuni ya ranchi ya taifa (NARCO) eneo la Misenyi kwa ajili ya ufugaji wa kisasa na wa kibiashara.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na katika tukio hilo mwananchi mwingine aliyetajwa kwa jina la Thomas Kasimbazi amejeruhiwa kwa risasi na wananchi wamewajeruhi walinzi watatu wa kitalu namba 20, kufuatia tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi wa mkoa wa Kagera Kamishina Msaidizi Mwandamizi Augustine Ullomi amefika kwenye eneo la tukio na kuzungumza na wananchi wa kitongoji cha Rwenkuba walioelezea juu ya tukio hilo ambapo ameahidi kuwa serikali itachukulia hatua kali wale wote watakaobainika walihusika na tukio hilo. 

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denis Mwila kuwapa pole ndugu na jamaa wa mwananchi aliyepoteza maisha amewaondoa wasiwasi wananchi kwa kuwaeleza kuwa serikali imeanza kutekeleza mikakati yake ya kuimarisha masuala ya usalama kwenye maeneo ya mipaka ili iweze kudhibiti vitendo vya uingizwaji holela wa mifugo toka nje vinavyofanywa na wananchi wasio waaminifu ambavyo vinachangia migogoro, ametoa kauli hiyo baada ya Charles Francis mwenyekiti wa tawi la Bubare la Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuiomba serikali iwahakikishie usalama wananchi hao.