Back to top

Mwarobaini wa ndoa hewa Dar es salaam kupatikana.

12 August 2019
Share

Serikali ya mkoa wa Dar es SSalaam imesema baada ya  mkutano wa 39 wa Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC wa wakuu wa nchi 16 na wanachama watatumia fursa hiyo kupata  uzoefu kutoka kwa nchi wanachama  ili kuona namna ya kupunguza wimbi la udanganyifu kwa kinadada kuahidiwa ndoa hewa ili wananchi wawe na mahusiano bora  na kupunguza watoto wa mitaani.

Aidha imesema pia kuna uwezekano wa kutaka ndoa zisajiliwe kwenye ofisi za mkoa pindi pale mwanadada akichumbiwa aingie kwenye ‘data base’ ya mkoa kupata uhakika wa taarifa kamili za mwenza wake.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw Paul Makonda.