Back to top

Mwenyekiti wa kitongoji achomwa na Singe ya Bunduki na askari Polisi

26 February 2020
Share

Mwenyekiti wa ulinzi wa kijiji cha Peramiho A mkoani Ruvuma ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mtakuja Pastorius Mbuya amejeruhiwa kwa kipigo cha askari polisi  waliochukizwa na mwenyekiti huyo kumpigia simu mkuu wao wa kazi na kuwagongea usiku wakati kituo cha polisi kimefungwa.
 
Bw.Mbuya alienda kituoni hapo saa sita usiku akiwa na kijana ambapo polisi walikataa kumshughulikia baada ya kukuta kituo cha polisi kimefungwa  hivyo kitendo cha kugonga kiliwachukiza askari hao ndipo wakampiga na kumchoma singe ya bunduki mguuni na mkononi
 
Dereva wa boda boda Alifa Ausi  aliyempeleka Bw.Mbuya kituo cha polisi kushughulikia  suala la mwanafunzi anasema alishudia polisi wakimtukana matusi  mwenyekiti wa kitongoji kabla ya kumpa kipigo kilichomjeruhi

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema atalifuatilia suala hilo na kuchukua hatua kwa kuwa linaondoa imani ya jeshi la polisi kwa wananchi
 
Akizungumza kwa simu kamanda wa polisi wa mkoa wa ruvuma ACP Simon Marwa amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa liko kwenye uchunguzi