Back to top

Mwili uliozikwa jana wafukuliwa na kubakwa Pugu.

12 April 2019
Share

Mwili wa aliyekuwa Afisa Madini Mary Mkwaya uliozikwa jana wafukuliwa na kudaiwa kubakwa Pugu Dar es Salaam na watu wasiojulikana ambao walibomoa  kaburi lake eneo la Pugu Mwakanga kisha kuvunja jeneza .

Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo kwenye makaburi ya roma eneo la shule ya sekondari Pugu.

kaka wa marehemu Bw Waziri Ngambeki amesema alipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa fundi aliyejenga kaburi hilo ambaye alienda kwa lengo la kumwagilia maji , na walipofika na kukuta kaburi la dada yake  Mary Mkwaya limebomolewa upande mmoja na na kuvunjwa jeneza na kukuta mwili ukiwa juu ya jeneza hali inayowashangaza hadi sasa.

Mwenyekiti wa mtaa huo wa Pugu Bombani Bw, Gido Berbard amesema ofisi yake ilipigiwa simu na ilipofika ilikuta hali hiyo ambayo haijawahi kutokea na baada ya kushuhudia iliwataarifu waliotoa kibali ili  kuuzika upya mwili huo.

Marehemu Mary Mkwaya aliefariki juzi alizikwa jana jioni saa kumi na moja ambapo usiku wa kuamia lero ndipo lilipotoea tukio hilo.