Back to top

Mwili wa aliyekuwa mtangazaji DW Isaac Gamba unafanyiwa uchunguzi

20 October 2018
Share


Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Dw, Isaac Gamba bado upo mikononi mwa polisi na madaktari wakichunguza chanzo cha kifo chake.

Gamba alikutwa amekufa nyumbani kwake baada ya kutoonekana kazini kwa siku mbili.

Mpaka sasa Polisi hawajatoa taarifa zozote  na inaelezwa kuwa huenda jioni ya leo kukapatikana taarifa toka Polisi. 

Gamba kabla ya kujiunga na DW radio alikuwa mtangazaji wa Radio One na ITV, 

Msiba wa Gamba unaelezwa kuwa uko eneo la Gongo la Mboto kwa shangazi yake.