Back to top

Mwili wa Mzee Mkapa waagwa Kitaifa Uhuru.

28 July 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Julai, 2020 amewaongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa aliyefariki dunia tarehe 23 Julai, 2020.

Mke wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Benjamin Willian Mkapa, Mama Anna Mkapa (aliyejivunikakitambaa cheusi)  akiwa na Wanafamilia baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, wakiwa wamesimama wakati wa kuwasili kwa msafara  uliochukua mwili wa Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla.