Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Subira Mgalu amekataa kuwasha umeme wa REA katika vijiji vitatu vya halmashauri ya singida ,kufuatia miradi hiyo kuonekana kasi yake ya kuweka nyaya ni ndogo hadi sasa ni nyumba moja tu ndiyo iliyo unganishwa umeme kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitano .
Mheshimiwa Mgalu ametoa uamuzi huo kufuatia malalamiko ya kucheleweshewa kuunganishiwa umeme licha ya wananchi kuweka miundombinu ya nyaya kwenye nyumba zao.