Back to top

Naibu Waziri apiga marufuku uchomaji matofali kwa kutumia kuni.

12 December 2018
Share

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  amepiga marufuku uchomaji matofali  kwa kutumia  kuni  katika maeneo ya mijini na  badala yake kushauri matumizi ya   pumba kufanyia akzi hiyo.
 
Mh. Kanyasu  alipozungumza na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Geita.
 
Amesema uchomaji matofali kwa kutumia nishati ya kuni umekuwa ukichangia  upotevu mkubwa  wa misitu hali inayotishia sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa.