Back to top

Naibu Waziri asitisha ugawaji wa hati za kimila 22,000 zilizoghushiwa.

10 June 2018
Share


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh.Angelina Mabula amesitisha uandikishaji na ugawaji wa hati za kimila 22,000 kwa ajili ya umiliki wa ardhi kwa wananchi wa vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Mbinga baada ya kubaini zimeandaliwa kinyume cha utaratibu huku pia sahihi ya afisa ardhi mteule wa wilaya hiyo, bi. Clementina komba iliyosainiwa katika hati hizo ikiwa imeghushiwa.
 
Mh. Angelina Mabula ametoa agizo mara baada ya kutembelea Ofisi ya Ardhi ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma na kushuhudia hati 22,000 za kimila ambazo ziliandaliwa kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi zikiwa zimeandaliwa kinyume cha utaratibu bila maeneo husika kupimwa na kuweka bayana matumizi bora ya ardhi.
 
Tatizo lingine kubwa alilolibaini Naibu Waziri wa ardhi,ni kughushiwa kwa sahihi ya afisa mteule wa ardhi wa wilaya ya Mbinga,Bi.Clementina komba na kupachikwa katika hati hizo.
 
Hata hivyo Afisa ardhi huyo Mteule wa wilaya ya Mbinga,Bi.Clementina anasema alishatoa ushauri wa kitaalamu katika vikao pamoja na kumshauri Mkurugenzi wake wa halmashauri.