Back to top

Naibu Waziri wa Ardhi akiri kukwama kwa ujenzi wa mji mpya wa Kawe.

07 May 2021
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angelina Mabula amekiri kukwama kwa ujenzi wa mji mpya wa Kawe kutokana na uhaba wa fedha ndani ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) baada ya shirika hilo kufikia kikomo cha kukopa cha idhini ya kukopa kilichowekwa na serikali kwa mradi husika.
.
Dk. Angelina Mabula amesema hayo wakati akijibu swali la  Mh.Halima Mdee mbunge alipotaka majibu ya serikali juu ya sababu za kukwama kwa mkakati wa ujenzi wa mji mpya wa Kawe.

Aidha, Naibu Waziri ameongeza kuwa mradi huo ulikwama kwa muda sasa unatarajiwa kuanza tena katika bajeti ya 2021/2021.