Back to top

Nchemba:Serikali imesikia kilio cha wananchi kuhusu tozo za miamala.

19 July 2021
Share

Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema Serikali imesikia kilio na maoni ya wananchikuhusu tozo mpya ya miamala ya simu na kuwaomba wawe watulivu wakati jambo hilo linatafutiwa ufumbuzi.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari akiambatana na Waziri wa Teknolojia ha Habari na Mawasiliano Dkt. Faustine Ndugulile.

Alisema kuwa jambo la tozo za miamala linatekelezwa kupitia sheria iliyopitishwa na Bunge lakini kuna kanuni za utekelezaji zinazo mhusu yeye kama Waziri wa Fedha na Mipango na maeneo mengine yanahusu Wizara ya Teknollojia ya Habari na Mawasiliano ambazo zitajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Dkt. Nchemba alisema kuwa siku ya Jumanne tarehe 20 Julai, 2021 kutakuwa na kikao kilichoitishwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, kujadili suala hilo na pia kutakuwa na kikao kingine cha Mawaziri wa Wizara zote kuchambua kwa kina suala hilo.

Dkt. Nchemba aliwaonya wale ambao wana nia mbaya ambao mara zote wapenda kupotosha ama kubadili dhana ya maana halisi ya jambo ambavyo lilikuwa limekusudiwa na kuwataka wasifanye hivyo, kwani mambo haya yana maslahi mapana kwa nchi.


Alisema tayari aliwapa maelekezo wataalam wa mifumo kuangalia vipengele vya Sheria ya mifumo ya malipo Serikalini pamoja na Sheria ya Mawasiliano ya Mtandao (EPOCA) inayoelezea kuhusu masuala ya miamala kwa njia ya mtandao na kuja na mapendekezo yatakayosaidia kufikia muafaka wa jambo hilo.

Kwa upande wake Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Dkt. Faustine Ndugulile alibainisha kuwa Wizara yake pia ambayo inaguswa moja kwa moja na tozo hizo imeendelea kupokea maoni na kuchakata taarifa mbalimbali tangu tozo hiyo ianzishwe na kumwahidi Waziri wa Fedha na Mipango kwamba atampa ushirikiano kuhakikisha kwamba maelekezo yaliyotolewa na viongozi yanatekelezwa.