Back to top

Ndalichako:Wafichueni watu wanaosambaza dawa za kulevya mashuleni.

16 October 2018
Share

Walimu kwa kushirikiana na  wazazi nchini waagizwa kuwafichua watu wanaosambaza dawa za kulevya katika baadhi ya shule za sekondari na vyuo na kuwauzia wanafunzi.

Serikali imewaagiza walimu na wazazi nchini kuwafichua watu wanaosambaza dawa za kulevya katika baadhi ya shule za sekondari na vyuo kwa ajili ya kuwauzia wanafunzi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kufuatia baadhi yao katika shule za sekondari kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu,sayansi na teknolojia Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako katika kongamano la wadau wa elimu lililofanyika wilayani Pangani kufuatia mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Issa kubainisha kuwa shule ya sekondari Funguni wanafunzi zaidi ya 10 wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Katika kongamano hilo wadau wa elimu wa shule za sekondari wilayani Pangani wamemueleza Mheshimiwa Waziri Ndalichako kuwa wapo baadhi ya watendaji wa serikali za vijiji,askari pamoja na wataalam wa afya kuwa wanashirikiana na baadhi wazazi kuwaficha watuhumiwa wanaowapa mimba wanafunzi bila kufikisha mashauri hayo katika vyombo vya sheria.