Back to top

Ndumbaro amtumbua Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Utalii Tanzania.

10 April 2021
Share

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Damas Ndumbaro amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Devotha Mdachi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Dkt.Ndumbaro amesema uamuzi huo umefanywa na bodi kwa kushirikianan na wizara, baada ya kugundua kuna ubadhirifu pamoja na tatizo la kiutwala, hasa rasilimali watu katika wizara hiyo.

Wakati huo huo, Dkt.Ndumbaro amemteua Betrida James ambaye ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi na Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kukaimu nafasi hiyo uchunguzi unapoendelea.

Aidha, ameiagiza bodi iwasimamishe kazi wafanyakazi wengine waliohusika na ubadhirifu huo, ili kupisha uchunguzi agizo ambalo Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.Thomas Mihayo amesema ataanza kuyafanyia kazi mara moja maagizo hayo ya Waziri.