Back to top

NEC yatangaza ratiba ya uchaguzi jimbo la Babati mjini na Ukerewe

18 October 2018
Share

Uchaguzi katika majimbo manne na kata 47 unatajiwa kufanyika desemba 2 mwaka huu baada ya wawakilishi katika maeneo hayo kuhama vyama na nafasi nyingine za udiwani kuachwa wazi kwa sababu mbalimbali.

Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salum Mbarouk ametangaza majimbo mawili na kata 26  leo ambayo ni Babati Mjini lililopo Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara na Jimbo la Ukerewe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza

Awali Nec iliyatangaza majimbo  ya Serengeti na  Simanjiro  na kata 21 kuwa wazi hivyo uchaguzi wa majimbo na kata zilizotajwa utafanyika siku moja.