Back to top

NEC yatangaza tarehe ya kuchukua fomu za urais, ubunge na udiwani.

23 July 2020
Share

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza rasmi tarehe 5 mwezi wa 8 ndio itakua siku ya kuanza kuchukua fomu za wagombea wa urais,ubunge na udiwani katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu huku ikitangaza kubadili majina kwa majimbo 3 ya uchaguzi hapa nchini.

Akizungumza jijini Dodoma Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema kutokana na mchakato wa upatikanaji wa wagombea urais, ubunge na udiwani zoezi la kuchukua fomu litaanza mwezi ujao.