Back to top

NEC yawataka wasimamizi wa uchaguzi kufuata Sheria.

17 October 2020
Share

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe.Jaji (mst) Semistocles amewataka watendaji wa uchaguzi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha kwamba kwenye Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, Sheria, Kanuni na Taratibu zinafuatwa.  

Kaijage ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Watendaji wa Uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam. 

Mkutano huo uliwaleta pamoja Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Maafisa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata, Mkutano kama huo umefanyika kwenye vituo saba (7) nchi nzima.