Back to top

NECTA YAKIRI MWANAFUNZI KUBADILISHIWA NAMBA

25 October 2022
Share

Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), limethibitisha kuwa mwanafumzi wa darasa la 7 Iptisum Suleman Slim, alibadilishiwa namba ya mtiahani na uchunguzi umepelekea kugundulika kwa wanafunzi wengine 7 kubadilishiwa namba zao za mitiahani, na kuchukua hatua ya kuifungia shule ya Chalize Modern kuwa kituo cha mitihani ya baraza hilo.

Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof.Adolf Mkenda, amesema uchunguzi umebaini taarifa zilizotolewa na mwanafumzi huyo ni kweli.