Back to top

NEMC yaagizwa kutoa vibali vya tathmini ya mazingira kwa wakati.

11 August 2020
Share

Serikali imeliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) litoe kwa wakati vibali vya tathimini ya mazingira katika miradi ya maji inayoanzishwa.

Aidha, imeitaka Mamlaka ya Bonde la Ziwa Tanganyika isimamie sheria ili kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji ambavyo vimekuwa  vikisababisha athari za kimazingira.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba ametoa maagizo hayo wakati akizindua bodi ya tano ya Bonde la Ziwa Tanganyika.

Amesema kumekuwepo na ucheleweshwaji wa vibali hali inayosababisha miradi mingi kushindwa kuanza kwa wakati.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Rasilimali za Maji Prof.Hadson Nkotagu ameishauri serikali ihimize uwekezaji katika sekta ya maji kwa kuboresha teknolojia ya uvunaji wa maji, ili kukabiliana na upungufu wa maji ifikapo mwaka 2025.