Back to top

NHIF kuwachukulia hatua wanaotibiwa kupitia kadi za watu wengine.

11 July 2018
Share


Zimebainika changamoto kwa baadhi ya wateja wa  mfuko wa taifa wa bima ya afya kwenda kuwatibu ndugu zao ambao si wanachama  kupitia kadi zao na wengine wakienda kutibiwa  na kadi za ndugu zao hali inayoleta mkanganyiko mteja  anapofariki  huku kadi aliyonayo  ikisomeka jina la mtu mwingine.

Wadau wa  mfuko wa taifa wa afya (NHIF)  ambao ni waganga katika Zahanati,vituo vya afya na Hospitali wanaeleza changamoto wanazokumbana nazo katika kuwahudumia wateja wa naotibiwa kupitia bima ya afya ambao wana uelewa mdogo kuhusu mfuko huo

Kwa upande wake meneja  wa NHIF mkoa wa Ruvuma Bw. Abdiel  Mkaro anamesema mfuko huo utawachukulia hatua za kisheria wanaotibiwa kupiti kadi za  ndugu zao ilhali wao si wanachama wa mfuko huo huku akieleza mkanganyiko unaojitokeza  mteja anayeotibiwa kwa kadi isiyo yake anapofariki.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mbinga Bw.Cosmas Nshenye amewataka madaktari kutoa huduma nzuri kwa wateja wa bima ya afya.