Back to top

Nyuki wawapa hofu wanafunzi wa Kitumbili Singida.

06 July 2020
Share

Zaidi ya wanafunzi mia tano wa shule ya msingi Kitumbili  Halmashauri ya wilaya ya Makalama  mkoani Singida wameingiwa na hofu ya kuumwa na nyuki kufuatia makundi makubwa ya nyuki kulundikana kwenye miti na makenchi ya mbao ya madarasa.
 
Wanafunzi waliokutwa wamesema licha ya wao kusoma kwenye madarasa lakini wamekuwa na hofu ya kuumwa na nyuki hao.

Kwa upande  wake  Makamu Mwalimu Mkuu wa shule ya Kitumbili Bwana Stephano Nade amesema wameshatowa taarifa kwenye sekta husika wilayani ili kuweza kuwaondowa nyuki hao.