Back to top

Nyumba zaidi ya mia moja zazingirwa na maji Bukoba.

26 February 2021
Share

Mvua zinazoendela kunyesha  wilayani Bukoba mkoani Kagera zimesababisha nyumba zaidi ya mia moja kuzingirwa na maji kufuatia mitaro inayosafirisha maji kuelekea ziwa victoria  kubomoka na mingine kushindwa kupitisha maji hali inayopelekea  baadhi ya wananchi  kulazimika kuhama makazi yao.
.
Aidha, mkuu wa wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Deodatus Kinawilo,  amewataka watu waliojenga katika eneo la Nyamkazi na pembezoni mwa ziwa victoria kuchukua tahadhari ya kuhama  mapema kutokana na kina cha ziwa hilo kuongezeka na kusababisha, maji kupelekwa upande wa makazi ya wananchi.