Back to top

Nzige tishio wavamia mashamba ya wananchi wa Mtaa wa SUKITA Tabata.

29 November 2020
Share

Kundi kubwa la wadudu wanaodhniwa kuwa ni Nzige ambao hawajulikani wametoka wapi wamevamia mashamba ya wananchi Mtaa wa SUKITA Tabata Jijini Dar es Salaam.

Wadudu hao wamekula majani yote ya miti na kuendelea kufanya uharibifu na kuzua hali ya taharuki kwa wananchi kusambaa na kuvamia zaidi mashamba yao ya mahindi na mchicha wanayolima kwa kumwagilia.

Akizungumza na ITV Bi.Doto Rashidi ambaye mjumbe wa serikali ya Mtaa Buguruni unaojumuisha mtaa huo, amesema wadudu hao wanaodhniwa kuwa ni Nzige wamevamia katika bustani yake ya nyanya, lakini hakujua iwapo ni wadudu hatari na kuomba serikalim kupitia Wizara ya Kilimo kuchukua hatua ya kuwateketeza wadudu hao kabla hawajaleta athari zaidi.

ITV inaendelea na juhudi za kuwatafuta Maafisa wa Wizara ya Kilimo kitengo cha kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao ili kujua ni hatua gani watachukua katika kuwadhibiti na kuwateteza wadudu hao.