Back to top

Omar al-Bashir ashitakiwa kwa ufisadi.

14 June 2019
Share

Rais aliyeng'olewa madarakani nchini Sudan Omar al-Bashir amefunguliwa mashtaka ya ufisadi, akikabiliwa na mashtaka ya kuwa na fedha za kigeni, kurundika mali kinyume cha sheria na kutoa amri ya hali ya hatari.

Shirika la habari la nchini Sudan SUNA lililomnukuu mwendesha mashtaka wa serikali nchini humo.

Wachunguzi wamemkuta kiongozi huyo wa zamani na zaidi ya Euro milioni 100, Baada ya kuitawala Sudan kwa muda wa miaka 30, wanajeshi walimwondoa Bashir madarakani baada ya maandamano makubwa yaliyofanyika kwa miezi kadhaa.