Back to top

Oparesheni ya kudhibiti uhalifu Ilala kufanyika nyumba hadi nyumba.

19 September 2018
Share

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bi Sophia Mjema amesema watapiga kambi katika mitaa yote ya Vingunguti kwa kufanya operesheni nyumba hadi nyumba ili kudhibiti tatizo la vibaka wanaopora watu hususani akina mama na watu wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi vinavyolalamikiwa na wananchi wengi kwenye kata hiyo.

Bi Sophia Mjema ameyasema hayo katika mkutano wa wananchi  wakati akijibu mbalimbali na kuwataka kuorodhesha majina ya watuhumiwa wanaojihusisha na vitendo hivyo ikiwemo changamoto ya vibaka na ujambazi vinavyowakosesha usingizi katika maeneo yao ili hatua zichukuliwe.

Awali wananchi hao walielezea kero mbalimbali ikiwemo wafanyabiahara katika eneo la Machinjio wakitakiwa wahame bila kupatiwa eneo mbadala ukosefu wa mitaro mitaani usafiri na changamoto kubwa ya maji iliyoongoza kulalamikiwa na wananchi wengi katika mkutano huo.