Back to top

Panya wavamia na kuharibu mashamba Arumeru.

26 May 2020
Share

Wakulima wa baadhi ya kata za wilayani Arumeru mkoani Arusha wamelalamikia kuvamiwa na kundi la panya ambalo limeharibu  zaidi ya hekari 850 za mazao yao.

Wakizungumzia tatizo hilo baadhi ya wakulima wamesema licha ya kutumia dawa za kuua panya hao changamoto bado ni kubwa na  elimu zaidi matumizi ya viuatilifu inahitajika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Meru Bw.Emmanuel Mkongo na mtaalam kutoka Wizara ya kilimo Bw Mwangi Jubilant wamesema wameshaanza kuwakabili panya hao.Katika kata ya Malula panya wameharibu hekari 390 na  kata ya Majengo wameharibu hekari 370.