Back to top

Papa Francis afanya marekebisho ya sheria ya kanisa katoliki.

12 January 2021
Share

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni papa Francis Jumatatu amefanya marekebisho rasmi ya sheria ya kanisa hilo ili kuruhusu wanawake kuchukua majukumu zaidi kinyume na ilivyokuwa hapo awali.

Sheria hiyo mpya kwa jina la kilatino, SPIRITUS DOMINI au Roho ya Mungu inaruhusu wanawake kuhudumu kanisani kwa kusaidia makasisi. Hatua hiyo inaendana na ahadi aliotoa awali ya kufanya marekebisho kwenye kanisa katoliki ambalo kihistoria limekuwa likihudumiwa na wanaume.

Sheria hiyo inasemekana kuwa itaimarisha zaidi msingi wa kanisa pamoja na kuhusisha kila mmoja kwenye shuguli za uinjilisti ingawa papa Francis amesema kuwa jukumu la kuhubiri bado litabaki kwa wanaume.

VOA Swahili