Back to top

Papa Francisco atuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya MV Nyerere

21 September 2018
Share


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Papa Fransisco ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere. 

Katika salamu hizo kupitia kwa  Balozi wake nchini Baba Mtakatifu amewapa pole wote walioko kwenye majonzi na kuwapa  moyo  wanaotafuta ndugu ambao hawajapatikana.

 Amemuomba Mungu awajalie  baraka,nguvu na faraja wote walioguswa na msiba huo.