Back to top

Pasipoti za Kieletroniki kutolewa katika ofisi zote za uhamiaji.

11 June 2018
Share

Pasipoti za Kieletroniki za kusafiria kuanza kutolewa katika ofisi za uhamiaji mikoani kwa nchi nzima Julai mwaka huu  ikiwa na lengo la kuwapunguzia gharama wananchi  hasa wa mikoani kufuata pasi hizo makao makuu ya uhamiaji.
 
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini DKT.Anna Peter Makakala amesema hayo katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida,nakusema kuwa mkoa wa Singida wameshafunga vifaa maalumu vya kieletroniki vya kutolea pasi za kusafiria.