Back to top

Polisi mkoani Arusha wakamata dola bandia

23 March 2019
Share

Kikosi maalumu cha jeshi la polisi mkoa wa Arusha kimefanya operesheni na kufanikiwa kuwakamata wafanyabiashara wawili wakituhumiwa kuendesha zoezi la kutengeneza dola bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania milioni thelathini kwa lengo la kuwatapeli watalii wanaoingia nchini.

Akizungumza mara baada ya operesheni hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathani Shana anasema wameamua kuendesha operesheni nyumba kwa nyumba ili kubaini mtandao unaozalisha dola bandia na kuziingiza kwenye mzunguko wa fedha za kigeni wakilenga kutapeli watalii

Aidha kamanda Shana anasema operesheni hiyo ni endelevu huku akiwataka wakazi wa jiji la Arusha pamoja na makampuni ya kitalii kuwa makini na fedha hizo bandia.
Wakizungumzia operesheni hiyo wakazi wa jiji la Arusha wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuendesha msako huo .