Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Ruvuma mrakibu msaidizi wa polisi Salumu Morimori amesema jeshi hilo limeanza operesheni ya kuyaondoa magari mabovu barabarani kuboresha usalama barabarani huku wananchi wakipongeza operesheni hiyo na kutaka iwe endelevu.