Back to top

Polisi Ruvuma yatangaza kiama kwa wanaofanya biashara ya magendo.

25 January 2021
Share

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali limetangaza kiama  kwa wanaofanya biashara za magendo mipakani kwamba  litawafikia na kuwakamata.
.
Kiama hicho kimetangazwa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Simon Maigwa wakati akizungumzia operesheni ya kusaka magari yasiyolipa kodi inayofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa ardhini LATRA na TRA ambapo magari  zaidi ya 80 yamekamatwa.
.
Naye mkaguzi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa ardhini LATRA Bw. Masudi Juma amesisitiza kutumika kwa tiketi za kimtandao kwa magari yaendayo mikoani.
.
kwa upande wake afisa wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Lungu Msinza amewataka wafanyabiashara kulipa kodi bila shuruti.