Back to top

Polisi Songwe latolea ufafanuzi tukio la askari kumshambulia dereva.

14 January 2019
Share

Jeshi la polisi mkoani Songwe limetolea ufafanuzi tukio lililorekodiwa na kusambazwa mtandaoni likionesha askari wa usalama barabarani wakipigana na dereva wa gari kuwa kilichofanywa na askari ni kumdhibiti dereva kama wahalifu wengine.
 
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Yusufu Sarungi amesema tukio hilo lilifikia hatua ya kupigana kutokana na dereva huyo kupuuzia maelekezo ya mafisa wa usalama barabarani na kutoa lugha za matusi.