Back to top

Polisi wamnasa aliyetapeli watalii Sinza jijini Dar es Salaam.

11 July 2018
Share

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kutelekezwa watalii wawili raia wa Marekani na India katika moja ya hotel Sinza Jijini Dar es Salaam baada ya mtu mmoja raia wa Tanzania kuwatapeli kiasi cha dola elfu tano za kuwatembeza katika vivutio mbalimbali vya kitalii nchini.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Saalam Liberatus Sabas amesema mtu huyo raia wa Tanzania aliyejifanya kumiliki kampuni ya utalii alifanikiwa kuwatapeli kwa lengo la kuwatembeza na kuwa tayari ameshatiwa mbaroni huku akionya juu ya matukio hayo ambayo yanaweza kuuwa kabisa sekta ya utalii nchini.
 
Aidha Kamanda Sabas amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata shehena ya mabalo ya nguo na viatu vilivyoibwa jijini vyenye thamani ya milion mia sita huku watuhumiwa watano wa tukio hilo wakiendelea kushikiliwa.

Matukio hayo yameelezwa kuwa ni mwendelezo wa operesheni inayoendelea kufanywa na jeshi hilo lengo likiwa ni kumaliza matukio ya ujambazi jijini Dar es Salaam ambpo pia magari sita na watuhumiwa wakupora pochi kwa kutumia pikipiki wamekamatwa.