Back to top

Polisi wanaowakamata raia wasio na makosa waonywa

13 June 2018
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Mwigulu Nchemba amepiga marufuku askari wa jeshi la polisi kuwakamata watu wasiofanya makosa kwa kisingizio cha kumpata aliyefanya kosa na kusema ni wajibu wa jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kumpata muhusika katika njia ambazo wamefundishwa pasipo kuleta madhara kwa wengine.

Waziri Mwigulu ametoa marufuki hiyo bungeni mkoani dododma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa viti maalum Devotha Minja ambaye alihoji kitendo cha polisi kukamata wasiofanya kosa na kuwaweka mahabusu kwa madai kuwa mfanyakosa atajitokeza.