Back to top

Polisi yaua majambazi 2 wakati wa majibizano ya risasi Arusha.

19 October 2020
Share

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeua majambazi wawili wakati wa majibizano ya risasi na polisi katika eneo la Olkerian kata ya Moshono jijini Arusha.

Tukio hilo limetokea usikuwa kuamkia leo ambapo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo ACP Salum Hamduni ameeleza kuwa baada ya kuuawa majambazi hao walipekuliwa na kukutwa na silaha mbili aina ya Short Gun na Bastola zikiwa na risasi huku wenzao wengine watatu wakitokomea kusikojulikana.