Back to top

PROF.ASSAD akabidhi ofisi nakusema hakufanya uharibifu wowote.

05 November 2019
Share

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, anayemaliza muda wake Prof. Mussa Assad amemkabidhi ofisi CAG mpya Charles Kichere jinini Dar es Salaam.

Baada ya makabidhiano ya ofisi CAG Charles Kichere amesema atayalinda mapato kwa wivu mkubwa kwani anajua ugumu wa kukusanya mapato.

"Nimefanya kazi TRA najua ugumu wa kukusanya mapato, nimekuja kulinda mapato, tena nitalinda kwa wivu mkubwa sana, sitakuwa na simile kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya"-CAG - Kichere.

CAG Kichere amesema 'Kama kulikuwa na mahusiano hafifu atahakikisha anaimarisha mahusiano kati ya ofisi ya CAG na Bunge.

Kwa upande wake CAG aliyemaliza muda wake Prof.Mussa Assad amesema baada ya kukabidhi ofisi anahamishia majeshi kwenye kilimo kwani miezi miwili iliyopita alianza kuwekeza kwenye kilimo, hivi endapo watu wakimuhitaji atakuja. 

Prof.Assad amesema licha ya kupitia changamoto nyingi lakini hatosita kumpa ushirikiano wa kutosha CAG wa sasa pale utakapohitajika.

"Kazi ya CAG ni kusaini ripoti lakini ripoti unachukua kazi za watu wengi sana ambao waliifanya maeneo mbalimbali hapa Tanzania, kwa hiyo nukta yangu ni kuwatazama vizuri sana watu hawa." ameongeza Prof. Assad.

Kwa Muktadha huo sasa Prof.Assad amesema"Nimepokea ofisi hii kutoka kwa Uttoh miaka mitano iliyopita naamini sikufanya uharibifu wowote mimi naamini mabadiliko yanaweza kutokea, lakini yatokee kwenye namna ilivyopangwa vizuri.

Ameongeza kwa kusema 'Kama kuna yeyote nilimkosea kwenye utendaji wa kazi basi anisamehe na mimi kama kuna mambo alinikosea nimemsamehe'-Prof.Assad.