Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi,uzembe na usimamizi mbovu katika miradi mikubwa ya maji hapa nchini, waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa amekiagiza chuo cha maji kufundisha uzalendo, nidhamu na maadili ili kuondoa tatizo hilo.
WaziriMbarawa amesema hayo mjini Morogoro wakati akizindua bodi ya ushauri ya chuo cha maji ambapo akasema kumekuwepo na vitendo vingi vya hovyo vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa sekta ya maji hasa katika miradi inayoendelea hivyo kuisababishia serikali hasara kubwa.
Waziri huyo akatoa mifano ya wahandisi wazembe waliotaka kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha kwenye moja ya mradi kwa kufanya upembuzi wa hovyo, kwa kulazimisha gharama kubwa ya matumizi ya bomba kubwa la maji la chuma wakati kukiwa na uwezekano wa kuweka bomba la plastiki.