Back to top

Rais ateua Naibu Katibu Mkuu mwingine.

18 July 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Julai, 2020 amemteua Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Haji alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi.

Uteuzi wa Dkt. Haji unaanza leo tarehe 18 Julai, 2020 na anatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.