Back to top

Rais Dkt.John Pombe Magufuli aivunja bodi ya TEMESA

23 September 2018
Share

Kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 katika ziwa Victoria, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri imevunjwa kuanzia leo tarehe 23 Septemba, 2018 wakati kamati ya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.